Mkongwe kutoka unyamani TID amezitaka kampuni mbali mbali kutangaza na wasanii wakongwe kwa kuwa wao ndio mizizi iliyohangaika kuisimamisha misingi ya bongo fleva mpaka kuanza kuheshimiwa na makundi ya rika zote.
Mkongwe TID
Akizungumza na Planet Bongo ya East Africa Radio kuhusu heshima ya Bongo fleva kwa wakongwe, TID amesema wakongwe wengi hawapatiwi 'deal' za matangazo kama wasanii wa sasa ambao wengine wamekuwa wakionesha dharau bila kujua gharama waliyotumia kusimamisha heshima ya muziki.
"Makampuni yanayotoa hizi deal kwa wasanii wa sasa wanakosea kwa sababu wanatoa kazi mbaya na hawana vitu vya maana kama sisi wakongwe . Sisi pia tuna kazi nzuri ambazo zinaweza kuuza na pia tuna tambua jamii inataka nini ndiyo maana tulihangaika kutengeneza msingi mzuri wa muziki" TID alifunguka.