Our Feeds
#htmlcaption1

Saturday, June 10, 2017

habarimoto255

YAMOTO BAND KAMA WEUSI - ASLAY

Msanii anayeunda kundi la Yamoto Band kutoka Tanzania, Aslay ameweka wazi sababu zilizomfanya yeye kuamua kufanya kazi zake binafsi nje ya kundi.Msanii Aslay.


Aslay alifunguka hayo katika kipindi cha Friday Night Live na kusema kuwa wao wameamua kuwa kama walivyo wasanii wa kundi la Weusi ambapo msanii anaruhusiwa kufanya ngoma zake mwenyewe na huku bendi nayo ikiendelea kuwa na ngoma zake.

"Mkubwa Fella alitoa tamko akasema sasa hivi ni ruksa kila msanii kutoa nyimbo zake mwenyewe ukiachana na bendi, ila bendi itaendelea kuwepo, ni kama wanavyofanya Weusi msanii mmoja mmoja anafanya kazi zake na kwenye bendi pia yupo" -  Aslay.

Msanii huyo ameachia video zake tatu mfululizo  "Angekuona",  "Usiitie Doa" na "Muhudumu" ambazo zote zinafanya vizuri.

Subscribe to this Blog via Email :
Previous
Next Post »