Malkia wa filamu Bongo, Shamsa Ford ameweka wazi kumuonea wivu mahusiano ya muigizaji mwenzake, Jenipher Kyaka ‘Odama’ kwa kuyafanya kuwa na usiri mkubwa huku akipongeza na kusema ndivyo inavyopaswa mtoto wa kike kufanya kwenye mapenzi.
Tujifunze kusifiana tukiwa hai siyo mpaka mtu afe ndo umsifie..“naomba nitumie nafasi hii kukupongeza msanii mwenzangu.una vitu vingi vikubwa ambavyo wasanii wengi wa kike tunatakiwa kukuiga.la kwanza napenda bidii yako ya kufanya kazi.wewe ni mwanamke mpambanaji sana.Unajituma sana kiukweli na wala hukati tamaa”.
“Pia ni mtu ambae hata ukipata mafanikio siyo mtu wa kujionesha na wala huna mbwembwe.. . lakini kubwa kuliko vyote napenda unavyoweka mahusiano yako ya mapenzi private.sijawahi ona hata siku moja umempost sijui boyfriend na hicho ndo kitu kizuri kwa mtoto wa kike.mimi kwa upande wangu ningerudisha siku nyuma kipindi kile nipo single nisingempost au kumuweka wazi mwanaume yoyote niliyekuwa naye kipindi kile.Natamani mume wangu ndo angekuwa mwanaume wa kwanza kwa watanzania kumjua.Natamani wasanii wengi wa kike wangeiga mfano kwako. Misingi uliyojiwekea kwenye maisha yako ni mizuri sana dada yangu.Una HESHIMA na THAMANI kubwa sana..Hongera sana @jenniferkyaka”-Shamsa ameandika kwenye ukursa wake mtandaoni