Our Feeds
#htmlcaption1

Tuesday, June 6, 2017

habarimoto255

Mimi kumkalisha Young Dee na Dogo Janja ni kama ‘kifo’ – Young Killer



Young Killer yupo tayari kwa ajili ya kolabo na wasanii wenzake Young Dee na Dogo Janja

Rapper huyo amesema, endapo itatokea kazi hiyo atakuwa yupo tayari kufanya huku akidai ana uhakika wa kuwakalisha wasanii hao.
“Suala la kufanya na mayoung katika track moja linawezekana kabisa, na mimi binafsi nipo tayari kufanya. Lakini nifanye kazi itakayokuwa na maslahi ndani yake, siyo nikafanye kazi inawafaidisha watu mimi chochote sina mfukoni. Sasa hivi muziki ni biashara, endapo itatokea nipo tayari kwa sababu ni wadogo zangu wale kwenye kazi itakapotokea tu lazima nitawaadhibu,” Killer amekiambia kipindi cha Dj Show cha Radio One.
“Yaani suala la mimi kuwakalisha ni kama ‘kifo’ ni lazima. Sihofii katika hilo ila nahofia tu katika maslahi, kwa sababu nimeshafanya collabo nyingi hazina maslahi ndani yake,” ameongeza.

Subscribe to this Blog via Email :
Previous
Next Post »