Baada ya Rais Magufuli kuweka wazi kwamba hakuna mwanafunzi atakayerudi kurudi shule baada ya kupata ujauzito, Msanii Nikki wa pili amedai kwamba mabinti mjamzito anahitaji kupatiwa elimu pamoja na msaada wa kisaikolojia kwani bado wananyanyapaliwa.
Msanii Nikki wa Pili
Nikki ametumia mitandao yake ya kijamii kuzunguumzia suala hilo amabalo limeua mijadala tofauti tangu jana baada ya kauli ya Rais kutolewa jana alipokuwa Bagamoyo kwenye ziara yake, na kusema kuwa familia nyingi zimepoteza watoto kutoka na utoaji wa mimba.
"Huko uswahilini kwetu kuna familia zimebaki na makovu ya kuwapoteza watoto wao walipokuwa wakijaribu kuwatowa ujauzito ili kuwaepusha na unyanyapaa wa kijamii kusemwa na kuoneshwa vidole. tafiti zinasema hata kwa watu wazima nao mimba yingi nizile zisizo za kutarajia ndio mana mimba laki 5 hutolewa kila mwaka. so kama wao linawashinda vipi kwa watoto" Nikki aliandika.
Ujumbe wa Nikki kwenye ukurasa wa Twitter
Nikki amezidi kufunguka kuwa suala la kumnyima binti elimu bado litakuwa na changamoto hasa kusababisha malezi ya mtoto kudorora
"Mimi nadhani msichana mjamzito anahitaji kuelimishwa zaidi kulindwa zaidi na kupewa msaada wa kisaikolojia, maana kwenye jamii bado kuna unyanyapaa.......baba atafungwa jela, mama akifukuzwa shule mtoto atalelewa na nani? Hili swala linahitaji tafakari zaidi ndio mana jamii yenyewe haya mambo huwa hawaya peleki mahakamani tujiulize kwanini?
\
Ujumbe wa Nikki kwenye ukurasa wa Twitter
Pamoja na hayo Nikki ameongeza kwamba "Namkubali sana Rais wetu kwa mambo mengi mazuri na ana nia njema.....lakini hili la mimba sijui labda wazazi wenyewe watowe maoni yao.
Ujumbe wa Nikki kwenye ukurasa wa Instagram