Our Feeds
#htmlcaption1

Tuesday, June 6, 2017

habarimoto255

GAME NDIYO CHANZO CHA BIFU LA ALIKIBA NA DIAMOND

Mwimbaji staa wa miondoko ya Mduara ATamefunguka kwenye XXL ya Clouds FM na kudai kuwa aliwahi kushuhudia ugonvi wa Alikiba naDiamond ambao kwa mujibu wake ulianzia Uarabuninaye alikuwa shahidi.



AT amesema watu wengi wanakurupuka kuhusu ugomvi wa Alikiba na Diamond kwa kuwa alikuwepo Oman mwaka 2010 ambapo Alikiba na Diamondwalikuwa wanacheza Game chumbani kwake kwenye Hotel waliyofikia.

“Tulikuwa Oman kwenye Hotel moja. Tulikuwa na Show, sasa walikuwa wanacheza Game Alikiba na Diamond huku Alikiba akiwa amechagua Real Madrid na Diamond amechagua Barcelona. Alikiba akilikuwa amefungwa mbili, Diamond tatu.“Kwa hiyo Alikiba alikuwa nataka kupiga free-kick kwenye game Diamond akamsukuma Alikiba na Alikiba akastopisha game akamwambia kuwa mwanangu nilikuwa nakutafuta muda mrefu sana ikabidi mimi ninyanyuke sasa niwaamue.” – AT

Subscribe to this Blog via Email :
Previous
Next Post »