Our Feeds
#htmlcaption1

Friday, June 9, 2017

habarimoto255

WOLPER - KAZI KWANZA MAPENZI BAADAE

Mkali wa filamu za bongo Jacqueline Wolper amesema kuwa, japo wanaume wengi wenye pesa wamekuwa wakimsumbua kumtaka kimapenzi, haoni haja ya kuwa nao kwa kuwa anaamini ni wasumbufu na hawana mapenzi ya kweli.


Akizungumza na Star Mix, Wolper alisema, kutokana na upendo wa kweli anaojitahidi kumuonyesha mwanaume anapokuwanae kwenye uhusiano na kujikuta akiambulia maumivu, ameona bora aweke kando masuala ya mapenzi na kuwa`bize’ na kazi zake.

“Sina mpenzi kwa sasa nimeona bora niweke pembeni haya mambo nifanye kazi  zangu tu ndo muhimu, nikipenda hawa wanaonisumbua `now’ nitapenda na nitakuwa kimapenzi, lakini bado wote wanaonisumbua hakuna aliyefaulu kunishawishi niwe naye,” alisema Wolper

Subscribe to this Blog via Email :
Previous
Next Post »