Our Feeds
#htmlcaption1

Monday, June 12, 2017

habarimoto255

WEMA SEPETU NA GABO KUJA NA KISOGO

Malkia wa filamu Bongo Wema Sepetu, ameweka bayana ujio wa filamu fupi mpya ya “Kisogo” aliyofanya pamoja na muigizaji mwenzake Gabo Zigamba, itakayo weza kupatikana kwa njia ya mtandao.


Wema amebainisha hayo kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram kwa kuweka kionjo cha filamu hiyo pamoja na ujumbe huu.

“Asikwambie Mtu Kuigiza Raha bwaaana… Sema ndo uwe unajua sasa…. Sio tu unaigiza ili mradi…. Afu pia ujue kuitendea haki character yako… Maana ukishakaa mbele ya Camera unasahau kabisa kama wewe ni Wema Sepetu sijui Tz Sweetheart… Unaweka pembeni na unavaa uhusika wako unaotakiwa…. Sidhani kama nimewahi kuwaangusha… Tanzama best short Film kiganjani kwa kutumia simu popote ulipo kutana na @gabozigamba1@wemasepetu @millardyayo ndani ya #kisogoDondosha App ya Uhondo tv bureee. Mwaka Huu Mbona Kama Kuna Raha Nyingi.” aliandika Instagram.

Wawili hao kwa sasa wanafanya kazi kwa ukaribu zaidi baada ya miezi kadhaa iliyopita kuweka wazi ujio wa filamu yao ya pamoja itwaayo, ‘Heaven Sent’.


Subscribe to this Blog via Email :
Previous
Next Post »