Our Feeds
#htmlcaption1

Wednesday, June 7, 2017

habarimoto255

Godzilla na Wakazi watoana povu, Bill Nass ahusishwa

Wasanii wa muziki wa hip hop nchini, Godzilla na Wakazi wamekuwa wametupiana maneno katika mtandao wa Twitter  kwa muda wa zaidi ya saa moja, huku wakazi akidai Bill Nass anampa stress Godzilla.
Katika majibizano hayo makali kuna sehemu Godzilla alimuambia Wakazi, “piga mixtape zakooo zote, kwa show, napiga Lakuchumpa tu na Nataka naenda kulala,”. Wakazi akajibu, “Kumbe unajua nina mixtape kibao!! Uwezo wa kufanya kama mimi huwezi bila hit song nime perform Big Brother, Nominated Kora,”.

Wasanii hao waliendelea kujibizana, ikafika wakati Wakazi akamwambia Godzilla, “Mimi nipo Level za Fid Q sio zako, wote hatuna tiki (NA NI SABABU HATUJAOMBA) we are busy impacting the game not a social media.

Usijichekeshe hapa!! Yaani leo ndio ume confirm kuwa Billnass anakupa stress.. Eti “msaada tu” unataka kukodi majeshi?!,”. Karibia mwishoni mwa majibizano yao,  Godzilla aliandika, “Mwanaume mwenzio anapokushambuli kama mwanamke kuna tatizo,”.
Hizi ni baadhi ya Tweets zao .
 

Subscribe to this Blog via Email :
Previous
Next Post »