Our Feeds
#htmlcaption1

Tuesday, June 13, 2017

habarimoto255

BEN POL AKUTANA NA EBITOKE

Baada ya msanii wa RnB Ben Pol kuonana na mchekeshaji kutoka Timamu African Media, Ebitoke aliyefunguka kumpenda muimbaji huyo, Ben Pol amefunguka kuhusu ujasiri wa mchekeshaji huyo.



Muimbaji huyo alipost picha ya mrembo huyo (hapo juu) na kuandika “Watu wengi wenye mafanikio makubwa Duniani walishapitia hatua ya “Kutokueleweka” either na jamii zao au hata na watu wao wa karibu.

Usikubali kuyumbishwa kwenye Malengo uliyojiwekea. #Focus #Tuesdaymotivation ,” aliandika Ben.

Huwenda baada ya wawili hao kuonana, wameweza kuongea na kuelewana mpaka Ebitoke kufikia hatua ya kujiita Ebi Pol.

Ebitoke amekuwa akiandika katika mtandao wa Instagram kumpenda msanii huyo na kuamua kuwajibu baadhi ya watu kuwa yeye ni sealed na sio used, pia thamani yake sio makeup ya kichina.

Subscribe to this Blog via Email :
Previous
Next Post »