Our Feeds
#htmlcaption1

Saturday, July 8, 2017

habarimoto255

MOBETO AMCHOKOZA ZARI

Mrembo Hamisa Mobetto anazidi kuzichukua headlines tangu ilipojulikana kuwa ni mjamzito mpaka ujauzito wake kuhusishwa na Diamond Platnumz mpenzi na mzazi mwenzake na Zari The BossLady na raundi hii amepost picha akiwa Nairobi na kuandika Mama Dee..?

Wanasema mwenye macho haambiwi tazama..
A post shared by HamisaMobetto (@hamisamobetto) on 

Monday, July 3, 2017

habarimoto255

KAZI YANGU MPYA NA DIAMOND ITAWATOA KIJASHO MASHABIKI – SAIDA KAROLI

Msanii wa muziki wa asili, Saida Karoli amedai baada ya kupokelewa vizuri kwa wimbo wake ‘Urugamba’ anajipanga kuachia wimbo wake mpya akiwa na Diamond pamoja na Belle 9.



Muimbaji huyo amedai kibao cha ‘Urugambo’ amekitoa kama kifungua kinywa, badala yake watanzania watarajie kupata nyimbo kali mfululizo.

Saida anasema nyimbo zinazofuata ni zile alizoimba akiwashirikisha Belle 9 na Diamond Platinumz.
“Urugambo nimetoa kama zawadi kwa Watanzania, niliona nijitambulishe kama chai ya asubuhi, lakini watarajie mambo makubwa kwani hivi karibuni mimi na Belle 9 tutatoa kazi ambayo itawatoa jasho mashabiki wa muziki,” alisema Saida.

Pia muimbaji huyo amedai kwa sasa atahakikisha anaachia nyimbo nyingi kali ambazo zitamuweka vizuri katika tasnia ya muziki.

CHANZO BONGO5

Tuesday, June 27, 2017

habarimoto255

KUFA KWA KANUMBA SIO SABABU YA BONGO MOVIE KUFA - GABO

Msanii wa Filamu Tanzania, Gabo amesema si kweli tasnia ya filamu imeshuka baada ya kifo cha Steven Kanumba.
Image result for gabo zigamba
Muigizaji huyo ameeleza kuwa watu wengi wanaamini kutokuwepo Kanumba kumedhoofisha soko kutokana alikuwa wenye kuleta changamoto ambayo kwa sasa haipo.
“Sio kweli industry ipo vile vile, kwa hiyo jamaa alikuwa analeta changamoto kwa wacheza sinema wengi sana hivyo baada ya kuondoka ule ushindani ukawa umeshuka, hicho ndio kitu ambacho wanakikosa,” Gabo ameiambia Bongo Dot Home ya Times FM na kuongeza kuwa
“Lakini mimi nisema waendelee kuwa na mapenzi ya dhati ila wasiste kutoa malalamiko yao na kukosoa pale ambapo wanahisi pameenda tofauti kwa sababu changamoto za watu pekee ndio zinabadilisha.Tunajua hapo tunakosea inabidi tufanye hivi, kwa hiyo tunaenda tunabadilika kutokana na mawazo ya watu,” amesema Gabo.
Katika hatua nyingine Gabo amemuelezea muigizaji Wema Sepetu ni mtu wa namna gani katika ufanyaji kazi hasa pale walipokuwa wakishoot filamu yake mpya ‘Kisogo’.
“Ni dada mmoja ambaye yupo na utaratibu wake, ukiufuata na kuusikiliza utafanya nae kazi vizuri sana na atakuwa yupo poa sana. Ukiwa nje ya huo utaratibu unaweza kumuona ni msumbufu na ukamuona kero kwenye kazi,” ameeleza Gabo.

Monday, June 26, 2017

habarimoto255

RAYVANNY AKAMILISHA NDOTO ZAKE

Kushindwa kutumia fursa kwa kila nafasi unayoipata imeonekana ni dhambi kubwa kwa wasanii wa WCB. Hatimaye Rayvanny amekamilisha ndoto yake aliokuwa akiiota kwa muda mrefu.
Hitmaker huyo wa Zezeta, ambaye siku chache zilizopita alinyakuwa tuzo ya BET, amefanikiwa kukamilisha kufanya kazi na Jason Derulo kutoka Marekani.
Kupitia mtandao wa Instagram, Ray ameweka picha akiwa syudio na msanii huyo na kuandika, “God bless you my brother @jasonderulo its amaizing opportunity,am so grateful for that……… Toka Saa 8 Usiku amekaa na mimi hadi Asubui… Studio kulikua na Watoto wakaaaaaliiiii 😂lakini kawacha waondoke sababu walichoka kukaa studio yeye kabaki na sisi tu. Naamini kilichofanyika Mtakipenda. Thanks boss @afrikidd @babutale.”
Baada ya wasanii hao kukamilisha kazi yao hiyo walijumuika pamoja katika kucheza mchezo wa mpira wa kikapu ambapo Ray alijikuta akiambulia za uso kutoka kwa Jason. Wawili hao kwa mara ya kwanza walikutana nchini Kenya kwenye Coke Studio Afrika wiki chache zilizopita.
habarimoto255

TUWE WASAFI JAMANI - LULU

Muigizaji wa filamu nchini Tanzania, Elizabeth Michael maarufu kwa jina la Lulu ameoneshwa kukasirishwa na vitendo vya uchafu kwa baadhi ya waumini makanisani.
Elizabeth ‘Lulu’ Michael

Lulu amesema waumini wawapo makanisani na hata nje wanatakiwa kuzingatia usafi wa mwili na roho kwani kuna muda huwa wanasalimiana wanapokuwa kwenye ibada hivyo kama hawatazingatia usafi huenda ikaleta taabu katika kukamilisha misa au ibada.
Mnaowekaga Vidole Puani Kanisani,Hamjui kama kuna ule muda wa kupeana mikono au Mnatakaga kugundua nini? Tuwe Wasafi Wa Roho Na Mwili Pia,“ameandika Lulu kwenye ukurasa wake wa Twitter.
Hata hivyo mrembo huyo ameongeza kuwa kuna siku moja alimuona muumini mmoja akishika pua na leo ameamua kumpa makavu kwa kumuelimisha.
Wallahy kuna Mmoja alifanya hvyo Pembeni yangu leo Sijampa mkono bali Nimempa UKWELI,“ameandika Lulu
habarimoto255

Mkishindana na mimi nitawaacha - Alikiba

Msanii Alikiba amefunguka na kusema kuwa yeye katika muziki wake hakuna mtu anayeshindana naye na kudai ila kama kuna watu wanataka kushindana na yeye basi atawaacha na kuendelea na mambo yake.


Msanii Alikiba
Alikiba anasema katika maisha yake ya muziki hataki kuona mtu yoyote anamtoa katika njia yake, ndiyo maana watu ambao wanakuwa wakiongea ongea sana juu yake yeye na muziki wake hawapi nafasi, kwani anaamini akiwapa nafasi wanaweza kumtoa kwenye mambo ambayo yeye amekusudia kuyafanya hasa zaidi katika muziki wake. 
"Unajua kila binadamu ana tabia yake, kuna wengine wanajua kabisa kwamba wanakosea lakini wanafanya hivyo kwa sababu na wapo wengine wanakuwa wanaongea pasipokujua kama wanakosea, hivyo mimi kama msanii sitakiwi kusikiliza hivyo vitu sababu nakuwa na mipango na malengo yangu, hivyo sitaki mtu yoyote aniingilie kwenye mipango yangu  kwa hiyo ukiwafuata unaweza kujiangusha" alisema Alikiba 
Mbali na hilo Alikiba amesema yeye haangalii ushindani na wala hashindani na mtu
"Mimi siangalii ushindani na wala sishindani na mtu ila kama wapo wanashindana na mimi nitawaacha washindane na mimi lakini mimi sishindani ila naangalia malengo yangu na mipango yangu katika muziki" alimalizia Alikiba 
habarimoto255

Ben Pol avunja ukimya kwa Ebitoke

Msanii Ben Pol amefunguka ya moyoni baada ya kukutana kwa mara ya kwanza na mchekeshaji Ebitoke kwa kusema anaamini watu wengi wameoa ama kuolewa na watu wasiowapenda kwa sababu ya kushindwa kuelezea hisia zao.
Ben amebainisha hayo kupitia ukurasa wake wa instagram baada ya mchekeshaji Ebitoke kuonesha hisia za mapenzi katika mitandao ya kijamii kwa takribani majuma mawili hivi sasa.
"Hakuna kitu kizuri kama kujishusha na kukubali kujifunza pale unapoona kuna jambo zuri la kujifunza, ikiwa unampenda mtu au unatamani nafasi fulani, utajuaje kama unaweza kuipata hiyo nafasi au la ikiwa haujaiomba kwa muhusika ?. Naamini watu wengi sana wameoa ama kuolewa na watu wasiowapenda kwa sababu tu walipoteza nafasi za kuwaambia hisia zao wale wawapendao. Mwishowe walipokuwa tayari kuwaambia ikawa 'too late" aliandika Ben Pol.
Pamoja na hayo, Ben aliendelea kusema "Ikumbukwe humu duniani sisi sote tunapita na labda huyo mtu kesho hatokuwepo. Ebitoke umenifundisha jambo kubwa sana maishani, najua wengi walikubeza sana wengine walikuambia hautaweza hata kuonana na mimi laini huwezi amini mimi nimefurahi mno, kukutana na wewe na kuongea" alisisiza Ben Pol
Kwa upande mwingine Ben amesema amepata jambo kubwa sana kupitia Ebitoke na kuahidi kuyaishi maneno yake siku zote mwa maisha yake.