Our Feeds
#htmlcaption1

Tuesday, June 13, 2017

habarimoto255

WAMETUMIA VYA KWANGU NA MIMI NATUMIA VYA KWAO - SAIDA KAROLI

Muimbaji wa muziki wa asili, Saida Karoli amedai ametumia vionjo vya wimbo wa Diamond na Belle 9 kwenye wimbo wake mpya ‘Urugambo’ baada ya waimbaji hao kutumia vionjo vyake katika nyimbo zao zilizopita.


Diamond alitumia vionjo vya wimbo ‘Maria Salome’ wa mkongwe huyo kwenye wimbo wake ‘Salome’ na Belle 9 pia alitumia vionjo vya wimbo huo huo kwenye wimbo wake ‘Give It To Me’.

Saida amesema alitumia vionjo vya wasanii hao baada ya waimbaji hao kuvitumia vionjo vya wimbo wake huo.

“Walitumia vionjo vya wimbo wangu wakijua mimi nipo hai ndio maana na mimi nikachukua vyao kama walivyochukua vyangu, nikatengeneza muziki na namshukuru Mungu umepokelewa vizuri sana,” alisema Saida.

Muimbaji huyo amedai alishindwa kurudi kwenye muziki kwa muda mrefu kutokana na kukosa menejimenti ya kuusimamiwa muziki wake.

Subscribe to this Blog via Email :
Previous
Next Post »