Our Feeds
#htmlcaption1

Tuesday, June 13, 2017

habarimoto255

SIWEZI KULALA NA NJAA - IZZO BIZNESS

Msanii kutoka 'Green City' akiwakilisha kundi la The Amaizing, Izzo Bizness amedai hawezi kulala njaa kusubiri simu za promota kwa ajili ya show kwani kipaji anacho ndio maana anajiongeza zaidi mikoani.


Msanii Izzo Bizness amefunguka hayo baada ya maswali mengi kuzuka kwa nini hana 'show' nyingi Dar Es salaam kama mikoani, na kueleza kwamba muziki ni biashara yake hivyo hataweza kubweteka huku biashara yake inaharibika..

"Sikai kutegemea mpaka Promota anipigie simu kuhusu show maana hapo kuna kuna kuanza mazungumzo na kushushana bei, ila natengeneza mwenyewe najijua mikoa flani ndani ya  Tanzania nakubalika nachukua opportunity hiyo kutengeneza show hizo peke yangu na mwisho wa siku maisha yanaendelea.

Haipendezi msanii kama mimi nianze kupiga vizinga hadi vya vocha , Hata prof. Jay aliwahi kusema kama kipaji unacho kwa nini ufe na njaa, na ndivyo nifanyavyo mimi ", Izzo alifafanuaAidha Izzo ameongeza kwamba pamoja na changamoto kama kundi la The Amaizing wanazokumbana nazo amewataka wasanii waimbaji   wajipange sana kwani ujio wa Abella Music lazima uwatingishe kwenye game.

"Kwa sasa The Amaizing tuna changamoto ukizingatia Abella ni mgeni ndo anaanza kutengeneza mashabiki kwa hiyo na uhakika akishapata kile anachohitaji atakuwa moto balaa na nitoe angalizo kwa waimbaji siyo kwa kuwa-disrespect hapana ila ujio wa Abella lazima uwasumbue hivyo wajipnge sana", Izzo aliongeza.


Subscribe to this Blog via Email :
Previous
Next Post »