Our Feeds
#htmlcaption1

Wednesday, June 7, 2017

habarimoto255

Miss Tanzania Diana Edward kufuata nyayo za Wema Sepetu

Miss Tanzania 2016/7 Diana Edward ameweka wazi yupo mbioni kuingia katika tasnia ya uigizaji wa filamu nchini [Bongo Movie] kama alivyofanya aliyekuwa Miss Tanzania mwaka 2006 Wema Sepetu.

Mrembo huyo amesema lengo la kuingia katika uigizaji, nikutaka kubadilisha mtazamo wa Watanzania kuwa nchini hakupatikani filamu zenye ubora au hazipo habisa, na yeye atajikita katika uigiaji wa filamu za action.

“Kila kitu kipo tayari, nimeshafanya mazoezi sasa hivi nasubiria mambo yangu yakikaa sawa nianze kutengeneza. Napenda action movie kwa sababu am so addicted in action movie, staki kusema mengi sana kwa sababu nasubiria maamuzi kutoka kwa meneja wangu itakuwaje, kwa hiyo msubiri,” amekiambia kipindi cha Twenzentu cha Times FM.
“Mimi nilikuwa naigiza kuanzia muda mrefu ingawa sikutoa movie yoyote,” ameongeza.
.

Subscribe to this Blog via Email :
Previous
Next Post »