Our Feeds
#htmlcaption1

Friday, June 9, 2017

habarimoto255

HARMONIZE ANATARAJIA KUPATA MTOTO AFRICASTI

Msanii wa muziki kutoka WCB, Harmonize amedai anaomba Mungu kila kukicha mpenzi mpya mzungu ajifungue mtoto mwenye rangi nyeupe kama mama yake.


Muimbaji huyo hivi karibuni aliweka wazi ishu za ujauzito wa mpenzi wake huyo ambaye ni raia wa Marekani.Akiongea na 255 ya XXL ya Clouds FM Jumatano hii, Harmo amedai kuna asilimia kubwa mpenzi wake huyo kujifungua mtoto wa kizungu na sio mwenye rangi kama yake

.“Ngoja nikwambie kitu kuna kuzaa mtoto na kuna kuzaa mtoto wa kizungu ni vitu viwili tofauti,” alisema Harmonize.

 “Naenda Marekani mara moja si unajua mke wangu anatakiwa kusarifi kaniambia kuna ishu tunaenda kufanya sasa mimba ikiwa kubwa atazuiliwa kupanda ndege,”Muimbaji huyo ambaye aliachana na malkia wa filamu, Wolper, amekuwa mwenye furaha toa mpenzi wake huyo awe na mimba licha ya baadhi ya mashabiki katika mitandao ya kijamii kumtania kuwa amekuwa mshamba.

Subscribe to this Blog via Email :
Previous
Next Post »