Our Feeds
#htmlcaption1

Saturday, June 17, 2017

habarimoto255

BEEF SIO KITU KIZURI - COUNTRY BOY

Msanii wa Hip Hop, Country Boy amesema ni vema Wakazi na Godzilla wakamaliza tofauti zao mapema au kuhakikisha tofauti hizo zinabaki kwenye muziki tu na sio kuingilia mambo mengine.Rapper Country Boy amesema kitu wanachokifanya sio kibaya ila kinaweza kuwa kibaya kwanamna wanashughulika nacho kwani wananchi wanakipokea kwa picha tofauti.


“Mimi naona wanapeana vitu vizito kiasi kwamba vinaweza kumstress mtu mmoja au mwingine kutokana kwamba kila moja ana hasira zake, siwezi kujua ugomvi wao ulianzia wapi mpaka wakanza kupishana, kama ni beef mimi napenda ya musically. Nachohofia itaenda kufika hadi nyumbani halafu itakuwa mbaya kwa sababu huwezi kujua mtu ana mapokezi gani katika moyo wake kwa kile anachokisi,” amesema Country Boy.

“Mimi nashauri kama kweli wamedhamiria beef yao iwe hivyo, basi wai-control iwe ya music na wa-battle kwa ajili ya mistari tu kwa sababu wao ni kioo cha jamii, na mnapohamia katika upande wa pili watu wanawaangalia kwa kwa jicho la tatu,” ameongeza.


Subscribe to this Blog via Email :
Previous
Next Post »