Msanii wa muziki wa Bongo Flava Baby Madaha ameonekana kuumizwa na Vanessa Mdee kutajwa mara kwa mara mwenyewe kuwania tuzo za muziki za nje.
“Tunapeleka watu kuwania tuzo wengine hawana vigezo vya hizo tuzo, especially nazungumzia kwa madada kuna dada mmoja yaani kila tuzo anaendaga lakini ashindi kutokana na nini hana qualification za hizo tuzo,” amesema Madaha.Muimbaji huyo ameongeza kuwa sasa ni wakati wa wasanii kuacha kuwa na uteam kwani muziki wetu unahitaji ushindani na tusupport.